Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri |
TABORA
Serikali
ya Mkoa wa Tabora imemwagiza kuwakamata waliokuwa viongozi wa Chama cha Ushirika
cha Mibono na wale Tupendane kwa ubadhirifu wa mamilioni ya fedha za wakulima
na vyama hivyo.
Kauli
hiyo imetolewa wilayani Sikonge na Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa mkutano ambao ni sehemu ya
utekelezaji wa magizo ya viongozi wakuu wa kitaifa waliotembelea mkoa huo na
kuwaagiza kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi.
Amesema
kuwa viongozi wote wanaotuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za vyama
na wakulima na wale wakulima wa tumbaku waliotorosha tumbaku katika msimu wa
2013/14 watafutwe popote walipo na kukamatwa ili waweze kufikishwa Mahakamani
kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.
Awali
Mwenyekiti wa Kamati ya Ufuatiliaji Fedha za wakulima za Msimu wa 2013/14
Valerian Kaozya akitoa kero yao kwa Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa baadhi ya
wakulima wa Mibono AMCOS wapatao 441 wanadai zaidi ya shilingi milioni 966 toka
msimu huo.
Alisema
kuwa hali hiyo ilisababisha Chama hicho kuwa na deni kwa kushindwa kulipa deni
walikopeshwa na benki kupitia ushirika wao.
No comments:
Post a Comment