Friday, 8 September 2017

Tetemeko kubwa la ardhi laikumba Mexico.



_97714587_mexico_earthquake_08_09_17
Image captionTetemeko kubwa la ardhi laikumba Mexico
Tetemeko kubwa la ardhi la nguvu ya 8 katika vipimo vya richa limekumba pwani kusini mwa Mexico.
Kitovu cha tetemeko hilo lilitokea umbalia wa karibu milomita 100 kuisni magharibi mwa mji wa Pijijiapan katika kina cha kilomita 35, kwa mujibu wa idara ya hali ya hewa ya Marekani.
Onyo la kutoea tsumani limetolewa nchini Mexico, Guatemala, El Salvador, Costa Rica, Nicaragua, Panama na Honduras.
_97714204_914995f0-9ab0-4814-96a6-b1a927640366Haki miliki ya picha
Image captionTetemeko kubwa la ardhi laikumba Mexico
Tetemeko hilo lilisikika mji wa wa Mexico City ambapo watu walitoka manyumbani mwao kwenda barabarani.
Mgeni mmoja katika mji huo Luis Carlos Briceno, aliliambia shirika la Reuters, "sijawai kuwa popote pale ambapo ardhi ilisonga sana."
Umeme umeripotiwa kupotea sehemu za mji.
Hakuna onyo la tsunami lililotolewa pwani magharibi mwa Marekani.
Mexico kwa sasa inatishana na kimbuga mashariki mwa pwani yake.
Kimbunga hicho cha kiwango cjha kwanza kiko umbalia wa killomita 300 kusini mashariki mwa Tampico na kimepata kasi ya kilomita 140 kwa saa.
_97717910_16a09ede-be42-4896-be64-ae966fd11656Haki miliki ya picha
Image captionTetemeko kubwa la ardhi laikumba Mexico
Vifo vinne viliripotiwa katika jimbo la Chiapa nchini Mexico karibu na kitovu na vingine viwili katika jimbo la Tabasco.
Uharibifu mbaya uliripotiwa kusini mwa Mexico na magharibi mwa Guatemala.
Picha katika mitandao ya kijamii zilionyeshj nyumba zilozokuwa zimeporomoka katika mtaa wa Oaxaca na Jichitan ambapo ikulu ya manispaa iliharibiwa kabisa.
_97715417_5b251090-5a91-4000-8a88-9d4f5bb71c24Haki miliki ya picha
Image captionTetemeko kubwa la ardhi laikumba Mexico
Kituo cha kutuo onyo ya tsunami cha Pacific kilisema kuwa mawimbi ya tsunami yanaweza kufika urefu wa mita 3 juu ya viwango vya kawaida yanaweza kutokea pwani ya Mexico. Watu wameanza kuondolewa kutoka pwani ya jimbo la Chiapas.
Tetemeko la ukubwa wa 8.1 katika vipimo vya richa linashinda la mwaka 1985 ambalo lilipiga karibu na mji wa Mexico City na kusababisha vifo vya maelfu ya watu.
_97717911_4c14a798-8169-4110-a993-edf2ab0f0802Haki miliki ya picha
Image captionTetemeko kubwa la ardhi laikumba Mexico@habari na Bbc swahili

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...