Zoezi
la la utoji wa chanjo ya kuwakinga na maradhi ya Mapafu mifugo hususani ngombe
katika Kata ya Tongwe halmashauri ya wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi limeanza
rasmi katika kata hiyo
Akizungumza
katika zoezi hilo Kaimu Afisa kilimo na mifugo wa halmashauri hiyo Ailiki Shoo
amesema zoezi hilo ni maalumu kwa ajili ya kuwakinga wanyama hao na maradhi ya
mapafu ambayo huathiri mfumo wa upumuaji wa wanyama kama wasipopatiwa chanjo ya
ya ugonjwa huo.
Kwa
upande wake Afisa kilimo na mifugo wa Kata hiyo Bwana Lenatusi Haule amesema
zoezi hilo linaenda vizuri kwani wafugaji wameitikia kwa wingi kushiriki na
kuwaleta wanyama wao katika chanjo hiyo ili waweze kupatiwa chanjo ya kuwalinda
na homa ya mapafu
Zoezi
hilo litadumu kwa muda wa siku saba na litajumuisha vijiji vyote vya kata ya
tongwe kabla ya kuhamia katika kata nyingine katika halmashauri hiyo.
Chanzo:Poul
Mathius
No comments:
Post a Comment