Picha haihusian na Habari
Wananchi wametakiwa kujitoa na kutowaficha watoto
wenye ulemavu wa akili kwani kitendo hicho ni kuwanyima haki yao ya msingi ya
kupata elimu.
Mwalimu
wa shule ya Msingi Ikola kwa vijana wenye mahitaji maalumu ulemavu wa
akili Shabani Chaula amesema kuwa
watoto hao wanaweza kufanya vizuri kama watawezeshwa hususani katika sekta ya
elimu.
Aidha
amesema kuwa jamii bado imekuwa haina mwamko hususani katika kuwasaidia watoto
wenye ulemavu kwani wamekuwa wakiwaficha.
Mtoto
mwenye ulemavu ana haki ya kupata nafasi sawa ya elimu,kushiriki katika michezo
na mazoezi pale inapowezekana ili kumsaidia kufikia malengo yake ya maisha
kwani ana haki sawa na watoto wengine wasio na ulemavu.
Chanzo:Restuta Nyondo
No comments:
Post a Comment