Mabehewa manne ya Treni ya
mizigo iliyokuwa inatoka Katavi kuelekea Tabora yameacha njia na kuanguka
katika eneo la Shankala mkoani Katavi.
Afisa Uhusiano Shirika la
Reli Mohamed Mapondela amethibitisha kutokea kwa
ajali hiyo nakusema hakuna mtu aliyejeruhiwa wala uharibifu wa mali na
kinachoendelea sasa ni kutoa mizigo na kuweka sawa njia ya treni ili safari
iendelee.
Hata hivyo Bwana Mapondela
hakueleza sababu haswa zilizosababisha ajali hiyo lakini hii inaweza ikawa
imechangiwa na uchakavu wa njia hiyo ya treni
Reli hiyo inayotajwa kuwa ni miongoni
mwa reli kongwe zilizojengwa nchini miongo kadhaa iliyopita
No comments:
Post a Comment