Kiongozi wa upinzani
nchini Kenya Raila Odinga ametangaza kuwa hayuko tayari kushiriki marudio ya
uchaguzi mkuu wa urais nchini humo.
Bwana Odinga
amesema kuwa anataka kuwepo mikakati ya kisheria na kikatiba inayohitajika,
kabla ya yeye kukubali kushiriki uchaguzi huo.
Bwana Odinga pia anataka mabadiliko kufanyiwa Tume ya
uchaguzi nchini humo, ambayo imelaumiwa na mahakama ya juu kwa wa kuendesha
uchaguzi kwa njia ambayo haiukuwa nzuri ambayo ilisababisha kufutiliwa mbali
matokeo.
Jana Jumatatu
Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini Kenya ilitangaza kwamba uchaguzi mpya wa urais
nchini humo utafanyika tarehe 17 Oktoba.
Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati alisema
uchaguzi huo utashirikisha wagombea wawili pekee wa urais, Rais Uhuru Kenyatta
na waziri mkuu wa zamani Raila Odinga.
"Hakutakuwa
na uteuzi mpya wa wagombea wa urais katika uchaguzi huo upya. Waliopinga
matokeo ya uchaguzi kortini, Bw Raila Odinga na mgombea mwenza wake Stephen
Kalonzo Musyoka na mshtakiwa wa tatu Rais Uhuru Kenyatta na mgombea mwenza wake
William Samoei Ruto, watakuwa ndio wagombea pekee," taarifa ya bw
Chebukati ilisema.
Katika kufutilia
mbali matokeo ya uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti, Mahakama ya Juu
iliiwekea lawama Tume ya Uchaguzi.
No comments:
Post a Comment