Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron
ametoa mwito kwa Ulaya kuiwekea vikwazo vikali zaidi Venezuela.
Macron pia amezitaka nchi zinazoshirikiana
kibiashara na Venezuela kuchukua hatua kama hizo ili kuongeza mbinyo zaidi kwa
utawala wa rais Nicolas Maduro.
Macron amesema hatua hiyo
inafuatia uamuzi uliotolewa na mahakama nchini Venezuela wa kuutenga upinzani
kushiriki uchaguzi utakaofanyika mwezi April mwaka huu.
Akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari ambao pia ulihudhuriwa na rais wa Argentina Mauricio Macri,Macron
amesema ataunga mkono hatua hizo iwapo mataifa ya Ulaya yataona kuna haja ya
kuongeza vikwazo dhidi ya serikali ya rais Nicolas Maduro.
Rais wa Argentina Mauricio Macri
naye pia ameshutumu utawala wa kiimla chini ya Maduro na kutoa wito uchaguzi
ujao kufanyika katika mazingira huru na wazi.
Uamuzi uliotolewa Alhamisi wiki
hii na Mahakama ya Juu ya Venezuela ulisafisha njia kwa Maduro kushinda muhula
mwingine wa urais katika uchaguzi huo utakaofanyika April.
Chanzo :Dw Swahili
#Changia Danu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment