Saturday, 27 January 2018

Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu

MPANDA

Diwani wa Kata ya Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Mh.Willium Liwali ame mshauri Mkurugenzi mtendaji Manispaa ya Mpanda kutafuta mahali pa kuwaweka wafanyabiashara wadogo wadogo wapatao 200 wa kata hiyo waliokosa mahali rasmi pa kufanyia biashara zao.

Mh.Liwali amesema hayo kufuatia agizo la Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu kuagiza wafanyabiashara wote walio katika masoko yasiyo rasmi katika Manispaa hiyo kutakiwa kuondoka na kufanyia biashara zao katika masoko rasmi.

Kwa mjibu wa Diwani Liwali masoko yote ambayo wafanyabiashara hao wangehamia yakiwemo soko la Mpanda Hotel lililopo kata ya Majengo na soko la Kachoma lililopo kata ya Makanyagio yote yamejaa.

Wiki iliyopita,mamia ya wafanyabiashara wadogo wadogo wanaofanyia biashara zao katika machinjio ya ng’ombe Mpanda Hotel waliandamana mpaka kituo cha Radio Mpanda Fm wakipinga agizo la Mkurugenzi anayewataka kuondoka katika maeneo hayo yasiyo rasmi.

Kwa mujibu wa agizo la Mkurugenzi Michael Nzyungu, wafanyabiashara wote walio katika maeneo yasiyo halali kwa biashara walitakiwa wawe wameondoka mpaka kufikia Januari 22 mwaka huu suala ambalo mpaka sasa limeshindikana.

Chanzo:Issack Gerald 
#Changia Damu Okoa Taifa

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...