MPANDA
Wananchi Mkoa wa Katavi wametakiwa kujenga tabia ya kuitumia
mahakama kama Chombo cha kupatia haki kama kichocheo cha kuimarisha dhana ya
Utawala bora hapa Nchini.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mheshimiwa
Salehe Muhando wakati wa uzinduzi wa wiki ya sheria ambayo yameanza kuadhimishwa katika Viwanja
vya mahakama ya wilaya Mpanda.
Wafanyakazi wa mahamani wakiwa kwenye maandamano. |
Askali wa mkoa wa katavi wakiwa kwenye maadamano ya wiki ya sheria iliyozinduliwa jana |
Picha na wanafunzi wakiwa katika maandamano ya ufunguzi wa wiki ya sheria iliyozinduliwa jana katika maeneo ya mahakama ya wilaya ya mpanda. |
Kwa upande wake hakimu mkazi
mfawidhi wa mahakama mkoani katavi,MH OMMARY HASSANI KINGWELE amesema dhima
kubwa ya uwepo wa wiki ya elimu ya sheria ni kuhakikisha kuwa wananchi wote
wanapata uelewa wa sheria.
Madhimisho hayo ya sheria
mwaka huu yaliyo na kauli mbiu MATUMIZI YA TEHAMA KATIKA UTOAJI HAKI KWA WAKATI
NA KWA KUZINGATIA MAADILI Kilele chake kitakuwa tarehe moja mwezi wa pili na
Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mkuu wa mkoa wa katavi meja jenerali mstaafu
Rafael Muhuga.
Chanzo:Ezelina Yuda
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment