Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta |
NAIROBI
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza watu anaopendekeza waidhinishwe
kuwa mawaziri katika serikali yake mpya.
Mawaziri sita ambao walikuwa wanahudumu katika serikali yake muhula
uliopita wamevuliwa uwaziri na kuteuliwa kuwa mabalozi.
Bw.Dan Kazungu ambaye amekuwa waziri wa madini, amependekezwa kuwa balozi
mpya wa Kenya nchini Tanzania.
Miongoni mwa walioteuliwa kuwa mawaziri wapya ni mwanahabari mkongwe
Farida Karoney ambaye ameteuliwa kuwa waziri wa ardhi.
Bi.Monica
Juma ameteuliwa kuwa waziri mpya wa mambo ya nje kuchukua nafasi ya Amina
Mohamed ambaye amependekezwa kuwa waziri wa elimu.
Walati
huo huo Mawaziri ambao wameteuliwa kuwa mabalozi ni Judi Wakhungu (Mazingira)
anayekwenda Ufaransa,Cleopa Mailu (Afya) anayekwenda Umoja wa Mataifa mjini
Geneva,
Willy
Bett (Kilimo) anayekwenda India,Jacob Kaimenyi (Ardhi) anakwenda UNESCO-Paris na Hassan Wario
(Michezo) anakwenda Austria
Chanzo :bbc Swahili
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment