MPANDA
Tatizo la mimba za utotoni katika
kata Mwamkulu Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi limekuwa gumu kulidhibiti
kutokana na jamii inayoishi mahali hapo kuishi kwa kuhamahama.
Hali hiyo imethibitishwa na Afisa
Mtendaji wa Kata ya Mwamkulu Bw.George Iresha wakati akizungumza na Mpanda
Radio kuhusu namna wanavyodhibiti watoto wenye umri mdogo kupata mimba.
Aidha amesema kuongezeka kwa shule za
msingi na vituo shikizi vya kielimu katika kata ya mwamkulu imewapunguzia
mwendo mrefu watoto ambapo umbali mrefu kutoka nyumbani mpaka shule zilipo
zimekuwa zikitajwa kuwa miongoni mwa vyanzo vinavyochangia mimba za utotoni.
Kata ya mwamkulu yenye wakazi wapatao
elfu saba ikiwa na wakazi wanaojishughulisha na kilimo na ufugaji ni miongoni
mwa kata 15 za manispaa ya Mpanda.
Chanzo: Issack Gerald
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment