Friday, 26 January 2018

huduma za afya kuboreshwa Mkoani Kigoma shirika la Thamini uhai likiwa ni lengo kupunguza vifo kwa akina mama wajawazito na watoto


KIGOMA
Katika kuboresha huduma za afya Mkoani Kigoma shirika la Thamini uhai limejitolea dawa na vifaa tiba takribani aina 50 katika vituo vya afya 46 vyenye thamani ya shiling million 127 lengo likiwa ni kupunguza vifo kwa akina mama wajawazito na watoto.

Akizungumza katika makabidhiano ya vifaa hivyo dkt Bingwa wa magonjwa ya akina mama ya uzazi kutoka shirika la Thamini uhai Sande Dominick amefafanua lengo kuu la msaada huo na kuwataka watoa huduma kutumia dawa na vifaa hivyo kwa lengo lililokusudiwa.


Kwa miaka kadhaa sasa idadi ya akina mama wanaojifungulia katika vituo vya afya imeongezeka kutokaasilimia 38 hadi kufikia asilimia 60 yote ni kutokana na jitihada za mashirika binafsi,

Akimwakilisha Kaimu katibu tawala Mkoani Kigoma  muhandisi Aziz Mtabuzi, Dkt Lameck Mdengo ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake baada ya kupokea msaada huo ametoa shukrani Kwaniaba ya serikali na kutoa rai Kwa vituo hivyo kutumia msaada huo kama ilivyotarajiwa.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...