DAR ES
SALAAM
Serikali imesema ugonjwa wa ukoma bado
unaendelea kuwa tatizo huku ikizitaja wilaya 20 na mikoa 10 inayokabiliwa na
maambukizi mapya ya ugonjwa wa huo.
Akizungumza na wanahabari kuhusu
maadhimisho ya siku ya ukoma duniani yanayofanyika Januari 28 kila mwaka, Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine
Ndugulile amesema Takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania miongoni mwa nchi 22 zenye
wagonjwa wengi wa ukoma duniani.
Amesema kwa mujibu wa takwimu za Mpango
wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma za mwaka 2016, zinaonyesha idadi ya
wagonjwa wapya 2,047 wa ukoma waligunduliwa ambayo ni sawa na watu 4
kwa watu 100,000.
Dkt. Ndugulile ametoa wito kwa wananchi
watakao ona dalili za ukoma ambazo ni pamoja na kutokwa na mabaka kwenye ngozi,
uvimbe na maumivu kwenye mishipa ya fahamu na ganzi kwenye mikono, kujitokeza
hospitali kupata matibabu kwa kuwa hutolewa bure, badala ya kuendekeza Imani
potofu kwamba ugonjwa huo wa kurithi au kulogwa.
Mikoa inayokabiliwa na ugonjwa wa Ukoma
ni, Lindi, Mtwara, Rukwa, Pwani, Morogoro, Geita, Tanga, Tabora, Dodoma na
Kigoma. Kwa upande wa Wilaya ni Kilombero, Mafia, Pangani, Mvomero, na Masasi
Mjini.
Chanzo: Mo dewji blog
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment