Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako |
NJOMBE
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,
Profesa Joyce Ndalichako amewataka watu kuacha kupotosha kuhusu sera ya elimu
bure kwa kuwakataza wananchi kuchangia maendeleo ya elimu.
Prof. Ndalichako ametoa wito huo jana
Mkoani Njombe ambako yuko kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya elimu.
Alisema kuwa, waraka wa elimu namba
tatu wa mwaka 2016 na namba tano wa 2015 una ainisha kwamba wazazi na kamati za
shule zinaweza kujiwekea utaratibu kwa wanaotaka kuchangia vitu vya shule
ikiwemo chakula.
Prof.
Ndalichako alisema, serikali imekataza walimu kujikita katika kukusanya
michango ya hiari ya wazazi inayochangwa kwa sababu mbalimbali.
Chanzo: Mo dewji blog
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment