Picha ya matukio ya ujenzi wa shule ya Msingi Kayenze |
TANGANYIKA.
Shule
ya msingi Kayenze katika kijiji cha Kamilala kata ya Katuma wilaya ya
Tanganyika mkoa wa Katavi imepatiwa zaidi ya shilingi million 66 kutoka shilika la P4R kwa ajili ya ujenzi wa
Vyumba vinne vya madarasa ,ofisi ya walimu na matundu sita ya choo.
Hayo
yamebainishwa na Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando wakati akizungumza
na wadau mbalimbali wa maendeleo ya Elimu amesema halmashuri kwa kushilikiana na
baraza la madiwani kwa pamoja wamekubalina fedha hizo zielekezwe katika shule
hiyo kutokana na upungufu wa miundombinu ya madarasa uliopo shuleni hapo.
Naye
mwalimu mkuu wa shule hiyo Donatus Sixmund Komba amesema shule hiyo ina jumla ya
wanafunzi 1120 na vyumba vitano vya madarasa hali ambayo huwalazimu kufanya
mapokezano ya madarasa kwa wanafunzi hao katika kuwapatia elimu wanafunzi hao.
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando akishilikiana katika shughuli za ujenzi wa shule ya Msingi kayenze. |
Kwa
upande wake mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Vicent Kadogosa amesema wananchi
wamekuwa na mwitikio mkubwa katika kuunga mkono serikali kwa kujitolea nguvu
kazi katika kuhakisha miundombinu ya elimu inakuwa rafiki katika shule hiyo.
Katika
ziara hiyo wanachi wamejitolea vifaa mbalimbali vya ujenzi pamoja na pesa tasilimu
shilingi laki sita huku mkuu wa wilaya hiyo akichangia tofali elfu mbili katika
kuunga mkono ujenzi wa madarasa ya shule hiyo.
Chanzo:Mpanda Radio
No comments:
Post a Comment