TANGANYIKA
Halmashauri
ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi,imepokea zaidi ya shilingi Milioni 222 kutoka
shirika la kiraia la Equip Tanzania,kwa ajili ya kujenga na kuboresha
miundombinu ya shule zilizopo wilayani Tanganyika.
Afisa
elimu taaluma wa halmashauri hiyo Mwalimu Florence Ngua ambaye pia mratibu wa
mpango wa Equip Tanzania, amesema kiasi hicho cha fedha kitatumika katika shule
na vituo shikizi mbalimbali vya kielimu ikiwa ikiwemo eneo la uwekeza la
Luhafwe ambao wametengewa zaidi ya shilingi milioni sitini.
Aidha
mwalimu Ngua amesema,vituo vinne vya kielimu kati ya 28 vinavyotakiwa kujengewa
na kuboreshewa miundombinu ya majengo ya shule,vinatarajiwa kutumia fedha
zilizotolewa na Equip Tanzania kwa mwaka wa fedha 2017/2018.
Kwa
upande wake Afisa habari wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Bw.Sylivanus
Ntiyakenye ametoa wito kwa wakazi wilayani Tanganyika kujenga makazi yao katika
maeneo yaliyopimwa ili kushirikiana na serikali kuleta maendeleo.
No comments:
Post a Comment