DODOMA
SERIKALI
imetoa wito kwa vikundi vya wavuvi vilivyopo katika ziwa Tanganyika kupitia
Halmashauri zao kujitokeza na kuchukua ruzuku ya boti injini 24 zilizobaki kwa
ajili ya kuendesha shughuli za uvuvi wenye tija.
Kauli
hiyo imetolewa jana bungeni Dodoma na naibu waziri wa mifugo na uvuvi
Mh.Abdallah Hamis Ulega wakati akijibu swali la Mbunge wa Mpanda Vijijini
Mh.Moshi Suleiman Kakoso aliyetaka kujua ni lini serikali itawapatia
vitendea kazi wavuvi wadogowadogo.
Wakati
huo huo Waziri
Ulega amesema,kwa mwaka wa fedha Mwaka wa fedha 2015/2016 serikali ya awamu ya
tano ilitenga shilingi milioni 400 zilizonunua boti injini 73 ambapo kati ya
hizo injini 49 zilishachujkuliwa na vikundi vya uvuvi nchini kwa mtindo
wa ruzuku kupitia Halmashauri zao.
Kwa
upande wake Mbunge viti maalumu Mkoani Katavi Anna Lupembe amemwomba
wizara kufika katika maeneo ya Ikola,Karema,Kapalamsenga na maeneo
mengine yanayoendesha shughuli za uvuvi ili kusikiliza kero za wavuvi.
Katika
mwaka wa fedha 2017/2018 serikali imekwishatenga shilingi milioni 100 ili kuendelea
kusaidia vikundi vya uvuvi vitakavyokuwa vimeundwa hapa nchini.
Source:Bunge
No comments:
Post a Comment