MPANDA
IDARA ya maendeleo ya ustawi wa jamii
Manispaa ya Mpanda inaendesha semina kwa
watu wenye ulemavu ili kuwapatia elimu ya namna ya kujikwamua na umaskini.
Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya
watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Mkoani Katavi Issack Lucas Mlela amethibitisha hatua hiyo ambapo amesema semina
hiyo itakuwa dira ya kufanya shughuli za maendeleo na zenye tija.
Mwezi uliopita,SHIVYAWATA Mkoani
Katavi lilisikika likilalamika kusahaulika kwa watu wenye ulemavu katika fursa
za maendeleo hususani katika ugawaji wa mikopo kwa vikundi vya wajasiliamali
kutoka idara za maendeleo ya jamii.
Mkoa Wa katavi unakadriwa kuwa na
watu wenye ulemavu zaidi ya 2000 huku wakigawanyika katika makundi ya watu
wasioona,wenye usonji,ulemavu wa ngozi albino,ulemavu wa
viungo,kutosikia(viziwi) na wenye mtindio wa ubongo.
No comments:
Post a Comment