KATAVI
Kamanda wa polisi Mkoa wa katavi ACP
Damasi Nyanda ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi
dhidi ya watuhumiwa wa makosa mbalimbali wakati wanapowakamata.
Kamanda Nyanda ametoa wito huo wakati
akizungumza na wakazi wa kijiji cha Kalovya kata ya Inyonga ambapo amesema
suala la kuchoma moto watuhumiwa halikubaliki badala yake watuhumiwa wafikishwe
katika vyombo vya sharia.
Amesema zaidi ya watu wapatao 77
wameuawa wilayani Mlele kwa kipindi cha mwaka 2015 huku mpaka kufikia mwaka huu
kwa mujibu wa kamanda Nyanda watu wapatao 150 wameuawa kutokana na wananchi
kujichukulia sheria mkononi.
Kwa upande wa makosa ya
ubakaji,kamanda Nyanda amesema mpaka mwezi Juni mwaka huu makosa 46 ya ubakaji
yameripotiwa katika jeshi la polisi huku visa vya watu kujinyonga,kukutwa
wamekufa navyo vikionekana kuwa katika hali ya juu.
@habari na mwandish wetu Issack Gerald
No comments:
Post a Comment