MPANDA.
Baadhi
ya wamiliki wa viwanda vya mpunga maeneo ya mpanda hotel Katika manispaa ya
Mpanda Mkoani Katavi wameiomba serikali kuboresha miundombinu ikiwemo barabara
zinazoingia na kutoka viwandani ili kukuza uchumi wa viwanda.
Wakizungumza
na mpanda redio wamesema katika msimu wa mvua magari yanayopeleka na kuchukua mizigo
viwandani hapo yamekuwa yakikwama kutokana na miundombinu ya barabara kuwa
mibovu hali inayorudisha nyuma maendeleo ya viwanda.
Aidha
wameongeza kuwa ili kufikia Tanzania ya
viwanda lazima serikali itengeneze mazingira mazuri ambayo yatawavutia
wawekezaji wa viwanda kuendelea kufanya
kazi katika maeneo hayo.
Serikali
ya Awamu ya tano nchini Tanzania inayoongozwa na Rais John Magufuli imeweka
msisitizo katika viwanda ili kuinua uchumi wake.
Source Rebecca Kija.
No comments:
Post a Comment