MPANDA.
Vijana
mkoani Katavi wametakiwa kutumia fursa ya machimbo ya madini ya dhahabu
yaliyopo mkoani hapa katika kujiinua
kiuchumi.
Hayo
yamesemwa na baadhi ya wachimbaji wadogo wadogo wanaofanya shughuli hiyo katika
machimbo ya dhahabu yaliyopo katika
kijiji cha Dilifu Mjini Mpanda wakati wakizungumza na mpanda radio machimboni
hapo.
Katika
hatua nyingine wachimbaji hao wamewataka vijana kupuuza maneno ya baadhi ya
watu kuhusiana na kazi ya uchimbaji madini kwani migodini kuna shughuli
mbalimbali ambazo hazihatarishi maisha ya wachimbaji.
Licha
ya sehemu nyingi za wachimbaji wadogo wadogo kutokuwa rasmi, uchimbaji wa madini
ni moja kati ya sekta iliyoajiri vijana wengi mkoani Katavi
@Source Haruna Juma.
No comments:
Post a Comment