Maelfu watafuta makao baada ya tetemeko nchini Iran na Iraq.
Jitihada kubwa za
uokoaji zinaendelea baada ya tetemeko kubwa kukumba eneo la mpaka wa
Iran na Iraq na kuwaua zaidi ya watu 400 na kuwajeruhi zaidi ya 7,000.
Makundi ya uokoaji yanatafuta manusura waliokwamwa ndani ya vifusi vya majengo yaliyoporomoka. Tetemeko hilo la ardhi ndilo baya zaidi kutokea duniani mwaka huu. Watu
wengine walioawa walikuwa kwenye mji ulio magharibu mwa Iran wa
Sarpol-e-Zahab ulio umbali wa kilomita 15 kutoka mpaka na sehemu zingine
za mkoa wa Kermanshah. Hospitali kuu wa mkoa huo iliharibiwa vibaya na kusababisha ikubwe na matatizo ya kuwahudumia wagonjwa. Mwanamke mmoja na mtoto waliondolewa kutoka kwa vifusi wakiwa hai kwenye mji huo, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Iran. Majengo mengi katika mji huo yanaonekana kuporomoka. Huduma za maji na umeme zimekatwa katika miji mingine na baada ya majengo kuporomoka watu walilazimika kulala nje kwenye baridi.
Shirika
moja la utoaji misaada lilisema kuwa watu 70,000 wanahitaji makao baada
ya tetemeko hilo, na kuna ripoti kuwa maelfu ya watu huenda wakalala
nje kwa usiku wa pili.
Maafisa nchini Iran wanasema kuwa watu 413
wameuawa nchi humo. Baadhi ya wanajeshi na walinzi wa mpaka ni kati ya
wale waliouawa. Nchini Iraq watu 9 waliuawa kwa mujibu wa msemaji
wa shirika la msalaba mwekundu. Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini humo
ilisema kuwa watu 500 walijeruhiwa huko na tetemeko hilo lilisikika huko
Irbil, Sulaimaniya, Kirkuk, Basra na mji mku Baghdad. Maporomoko
yamefanya vigumu kwa waokoaji kufika maeneo ya vijijini na kuna hofu
kuwa huenda bwawa lilo huko likapasuka baada ya kuharibiwa na tetemeko
hilo. Watu wanaoishi karibuwametakiwa kuhama.. chanzo:Bbc swahil
No comments:
Post a Comment