Wednesday, 22 November 2017

Hamashauri ya Mpimbwe mkoani katavi imetajwa kufanya vizuri kitaifa katika ugawaji wa mikopo kwa vikundi vya akina mama na vijana



 
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali mstaafu Rafael Muhuga
MPANDA.


Hamashauri ya Mpimbwe mkoani katavi imetajwa kufanya vizuri kitaifa katika ugawaji wa mikopo kwa vikundi vya akina mama na vijana

Hayo yamebaishwa jana na mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali mstaafu Rafael Muhuga katika hafla ya ugawaji wa mfano wa hundi kwa vikundi 12 vya manispaa ya mpanda iliyofanika katika viwnja vya ofisi za kata ya Mpanda Hotel

Katika hafla hiyo mkuu wa mkoa amekabidhi hundi yenye jumla ya sh milioni 30 kwa vikundi vya akina mama na vijana 12 na sh milioni 7 kikundi cha Kashaulili Livestock Keeping.

Meja Jenerali Mstaafu muhuga amewaasa wanakikundi wote kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa na kuzirejesha kwa wakati ili ziweze kukopeshwa kwa vikundi vingine.
 
SOURCES:HARUNA JUMA.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...