Wednesday, 22 November 2017

Wizara ya fedha ya Marekani imetangaza kuweka vikwazo vipya dhidi ya kampuni kadhaa, meli na watu binafsi kutoka Korea Kaskazini, ili kukatiza zaidi biashara yanchi hiyo pamoja kuzuia vyanzo vya mapato.

Waziri wa fedha wa Marekani Bw. Steven Mnuchin

WASHGTON.

Wizara ya fedha ya Marekani imetangaza kuweka vikwazo vipya dhidi ya kampuni kadhaa, meli na watu binafsi kutoka Korea Kaskazini, ili kukatiza zaidi biashara yanchi hiyo  pamoja kuzuia vyanzo vya mapato.

Taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo imesema, Marekani itaendelea kuizuia Korea Kaskazini kupata fedha zinazotumika katika kuendeleza miradi ya silaha za nyuklia na makombora.

Waziri wa fedha wa Marekani Bw. Steven Mnuchin amesema, vikwazo hivyo vitaweka shinikizo zaidi kwa uchumi wa Korea Kaskazini.

Kwa mujibu wa sheria husika, mali za mashirika na watu binafsi waliowekewa vikwazo zilizoko nchini Marekani zinazuiwa, na raia wa Marekani hawaruhusiwi kufanya biashara na mashirika na watu hao.

SOURCES:CRI KISWAHILI.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...