Makamu wa zamani wa rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa |
HARARE.
Makamu wa zamani wa rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, anatarajiwa kuapishwa kuwa rais wa nchi hiyo Ijumaa wiki hii kufuatia kujiuzulu kwa rais Mugabe baada ya kuliongoza taifa hilo kwa karibu miongo minne.
Hatua hiyo inakuja huku Mnangagwa kurejea nyumbani leo hii, ikiwa ni wiki mbili tangu alipokimbia baada ya kufutwa kazi na Rais Robert Mugabe.
Hatua hii inakuja baada Mugabe kutangaza kujiuzulu wadhifa wa urais jana, na kuhitimisha utawala wake wa mabavu wa miaka 37.
Mmoja wa wasaidizi binafsi wa makamu huyo wa rais wa zamani, Larry Mavhima, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba Mnangagwa anarejea leo hii, na kuahidi kuwaarifu waandishi wa habari kuhusiana na kurejea kwake.
Hapo Jumapili, Mnangawa alichaguliwa kuwa kiongozi wa chama tawala cha ZANU-PF, akichukua nafasi ya Mugabe, na anatarajiwa kuapishwa kuwa rais wa mpito wa taifa hilo la kusini mwa Afrika.
SOURCES:DW KISWAHILI.
No comments:
Post a Comment