Wednesday, 22 November 2017

Balozi wa Oman Ali Al Mahruqi amesema Wafanyabiashara wa nchi hiyo wamevutiwa na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kujenga mazingira bora kwa wawekezaji.


Balozi wa Oman Ali Al Mahruqi na Makamu wa Raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu.


 DAR – ES SALAAM.

Balozi wa Oman Ali Al Mahruqi amesema Wafanyabiashara wa nchi hiyo wamevutiwa na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kujenga mazingira bora kwa wawekezaji.

 Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa  mazungumzo baina yake na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI) Joseph Kakunda na kuongeza kuwa suala la usalama wa mitaji yao ni jambo ambalo Wafanyabiashara hao wanapenda kuhakikishiwa na Serikali ya Tanzania.

Amefafanua kuwa miongoni mwa fursa zinazowavutia Wafanyabiashara wa Oman kuja kuwekeza nchini ni pamoja na ubora wa miundombinu katika sekta za elimu na mifugo ikiwemo upatikanaji wa  nyama.

Kwa upande wake Naibu Waziri Kakunda amemuahidi Balozi Mahruqi kufanyia kazi changamoto zilizopo ili kuhakikisha wawekezaji kutoka Oman wanakuja kwa wingi kuwekeza nchini bila ya kuwa na hofu ya usalama wa mitaji yao.

SOURCES:MO DEWJI.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...