MPANDA
Wafugaji katika
Halmashauri ya manispaa ya mpanda mkoani
Katavi wametakiwa kuzingatia ufugaji wa ndani ili kuondokana na
uharibifu wa mazingira.
Yameelezwa hayo na
Afisa mifugo na uvuvi wa halmashauri ya Mpanda Bwana Godfrey Tomasi wakati akizungumza katika kipindi cha kumekucha
Tanzania kinachorushwa na Mpanda Redio na amesema wafugaji wanatakiwa kujenga
mabanda kwa ajili ya mifugo yao ili kuepukana na mifugo kuzurura mitaani.
Kwa upande wa Afisa
Mazingira manispaa ya Mpanda Bwn Said Mwandua amesema wameanza kutoa elimu kwa
wafugaji juu ya ufugaji wa ndani na kwa atakaye kiuka atalazimika kulipa faini
ya shilingi elfu hamsini.
No comments:
Post a Comment