DAR ES SALAAM
Mtoto wa aliyekuwa mwanasiasa maarufu Tanzania Chacha Wangwe, Bob Chacha Wangwe, amehukumiwa kwenda jela mwaka mmoja na miezi sita au kulipa faini ya milioni 5 kwa makosa ya kimtandao.
Hukumu hiyo imetolewa na hakimu Huruma Shahidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam, na mshtakiwa kutakiwa kutekeleza moja ya adhabu hizo alizoambiwa.
Bob Chacha Wangwe anakabiliwa na makosa ya kimtandao kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa facebook kwamba 'Zanzibar inakandamizwa na Tanzania Bara na kwamba ni koloni lake'.
Sheria ya makosa ya kimtandao nchni Tanzania imeanzishwa mnamo sept 2015 ikiwa na lengo la kudhibiti matumizi mabaya ya mitandao hiyo.
Source-Mwananchi
No comments:
Post a Comment