Thursday, 16 November 2017

Umoja wa Afrika umeitaka serikali ya Zimbabwe na jeshi la nchi hiyo kutatua mgogoro wa kisiasa kwa kufuata katiba ya nchi hiyo.



ADIS ABABA

Umoja wa Afrika umeitaka serikali ya Zimbabwe na jeshi la nchi hiyo kutatua mgogoro wa kisiasa kwa kufuata katiba ya nchi hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki Mahamat amezihimiza pande zote kuheshimu katiba ya Zimbabwe na vifungu husika vya katiba ya Umoja wa Afrika.

Amesema umoja huo unafuatilia hali ya nchini Zimbabwe, na kuahidi kushirikiana na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC, ili kuhakikisha mgogoro wa kisiasa nchini humo unatatuliwa kwa njia ya amani.

Mpaka sasa wachambuzi wa masuala ya kisiasa wamekitaja kitendo kilicho fanywa na jeshi hilo kuwa cha kimapinduzi dhidi ya Muimla Robert Mugabe anayetajwa kuwa kiongozi mzee barani afrika.

SOURCE: CRI SWAHIL

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...