MANYARA
Wachimbaji wadogo mgodi wa Tanzanite katika
Mji mdogo wa Mirerani uliopo wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara, wameiomba
Serikali kuhakikisha nia ya kujenga ukuta unaozunguka mgodi huo inakuwa na
manufaa kwao, maendeleo ya Taifa.
Wakizungumza
katika kikao cha wadau wa madini ya Tanzanite, wachimbaji hao wamesema nia ya
kujenga ukuta isiwe kuwakandamiza na kuwagawanya.
Katibu
wa chama cha madalali wa madini mkoani Manyara, Mohamed Mughanja amesema
kwa miaka mingi wananchi wa Mirerani, wachimbaji wadogo wa Tanzanite na
madalali waliishi kwa kutegemeana hivyo ukuta huo usilenge
kuwatenganisha.
Mwenyekiti
wa chama cha wachimbaji wa madini Mkoani Manyara Sadiki Mneney amesema
wachimbaji madini wanapaswa kupewa ushirikiano wa kutosha baada ya kumalizika
kwa ujenzi huo.
Chanzo:mwananchi
Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment