Wednesday, 12 July 2017

DIWANI AITOSA CHADEMA AKIELEZA ANAMUUNGA MKONO RAISi MAGUFULI.

                                                         Solomon Laizer

Ni dhahiri sasa Chadema kanda ya kaskazini ipo njiapanda baada ya diwani mwingine kujiuzulu jana, huku hofu ya wengine zaidi kuchukua hatua kama hiyo ikiwa imetanda katika wilaya za Hai, Monduli na Arusha Mjini.
 Solomon Laizer, diwani wa Kata ya Ngobobo, amezidisha hofu hiyo baada ya kutangaza kujiuzulu wadhifa huyo wa kuchaguliwa na kujiunga na CCM, akidai kuwa amekunwa na utendaji wa Rais John Magufuli.
 Laizer alimkabidhi jana mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru, Christopha Kazeri barua yake ya kujizulu na kuwa diwani wa sita kutoka Chadema kujivua wadhifa wake kwenye mkoa huo ambao ni ngome ya chama hicho kikuu cha upinzani.

 Madiwani wengine ni Credo Kifukwe, aliyekuwa Kata ya Muriet, Anderson Sikawa (Legaruki)Emmanuel Mollel (Mikamba), Greyson Isangya (Mororoni) na Josephine Mshiu aliyekuwa wa viti maalumu.   Mwenyekiti wa Kanda ya kaskazini ya Chadema, Aman Golugwa amesema wamebaini mpango huo wa kuwashawishi madiwani wengine wa Chadema katika wilaya nyingine za Mkoa wa Arusha na Kilimanjaro.

 “Muda huu nipo Hai kuna mambo haya haya ya ajabu yanaendelea Golugwa. “Kuna taarifa kuwa kuna ushawishi unaendelea pia Monduli, Hai, Arusha Mjini na maeneo mengine,” alisema. Amesema wamelenga majimbo ambayo ni ngome ya Chadema, akitoa mfano wa Arusha Mjini ambako mbunge wake ni Godbless Lema, Hai ambako yuko Freeman Mbowe na Monduli ambako mbunge wake ni Julius Kalanga. Katika barua yake, Solomon amesema anamuunga mkono Rais Magufuli kwa kuwa anafanya kazi nzuri na kupata sifa ndani na nje ya nchi na amewaomba wananchi wa kata hiyo.

 Chadema ilishinda halmashauri 25 kati ya 26 za halmashauri ya Meru katika Uchaguzi Mkuu uliopita. Kata pekee iliyoenda CCM ni Ngarenanyuki na nafasi ya ubunge ilichukuliwa na Joshua Nassari wa Chadema.  Akizungumza jana, Kazeri amesema tayari amepata barua ya kujiuzulu kwa diwani huyo na taratibu zimeanza ili kutoa taarifa Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) ili kutangazwa uchaguzi mdogo.

Akizungumzia kujiuzulu madiwani watano katika jimbo lake, Nassari amesema madiwani hao wanashawishiwa kwa njia ambayo si sahihi, akisema suala hilo halina maslahi kwa umma. Nassari amesema walipata taarifa za mpango wa kujizulu kwa diwani huyo na walipomfuata alikiri akushawishiwa na CCM na kuwahakikishia kuwa angehama chama.

Hata hivyo, madiwani wanaohama wanapinga kuwa wameshawishiwa kufanya hivyo.Hadi sasa madiwani watano wa Chadema waliojiuzulu ni Credo Kifukwe wa Kata ya Murieti jijini Arusha.Wengine waliojiuzulu katika Jimbo la Arumeru Mashariki na kata zao kwenye mabano ni Anderson Sikawa (Leguruki), Emmanuel Mollel (Makiba), Greyson Isangya (Maroroni) na Josephine Mshiu (Viti Maalumu).

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...