MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imetangaza makusanyo ya kodi kwa mwaka wa fedha 2016/17 kuwa yalikuwa Sh trilioni 14.4.
Makusanyo hayo yana ongezeko la asilimia 7.67 ya makusanyo yaliyofanywa na TRA katika mwaka wa fedha wa 2015/16 ambayo yalikuwa Sh trilioni 13.3. Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Walipa Kodi, Richard Kayombo alisema kwa Juni ilikusanya kiasi cha Sh trilioni 1.37.
“Tunawashukuru wananchi wote ambao wametusaidia kukusanya kiasi hicho, kodi hizi ndizo zinazoiwezesha serikali kufanya shughuli zake za maendeleo,” alieleza Kayombo. Kayombo pia alisema mamlaka imeendelea kukusanya kodi mbalimbali ikiwemo kodi ya majengo na mwitikio wake umekuwa ni wa kiwango cha kuridhisha.
Alisema aliwashukuru wananchi wanaojitokeza katika ofisi mbalimbali za mamlaka nchi nzima ili kulipia kodi hiyo ya majengo ambayo mwisho wake wa kulipa ni Julai 15, mwaka huu.
mkurugenzi wa huduma na elimu kwa walipa kodi Bw. Richard kayombo
“Zimebaki siku nne tu za kulipia kodi hii, tunawaomba wananchi wajitokeze kulipia kodi hiyo,” alisema na kuongeza kuwa TRA imeboresha huduma katika ofisi zake kuhakikisha wananchi hawakai muda mrefu kwenda kulipia kodi hiyo.
Aliongeza kuwa TRA inatoa mwito kwa wafanyabiashara wote kutoa risiti za kielektroniki (EFDs) pindi wanapouza bidhaa au huduma na wananchi wote, kuhakikisha wanadai risiti pindi wanaponunua bidhaa au huduma katika maduka au sehemu wanazotoa huduma mbalimbali kumbuka kuchukua au kupokea risiti.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Featured post
MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO
Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio ...
-
NSIMBO Soko la Katumba Mnyaki linalomilikiwa na halamshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi halina choo tangu kuanzishwa kwake hali...
-
MLELE Shule ya msingi kusa iliyopo katika kijiji cha Kanoge kata ya utende Halmashauri ya wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi inatalajia k...
-
Mahindi MAHINDI yanaendelea kuwadodea wakulima mkoani Rukwa baada ya wafanyabiashara na watu binafsi kuchangamkia mahindi kut...
No comments:
Post a Comment