Wednesday, 12 July 2017
HATIMAE BODI YA MIKOPO KUWABANA WENYE VYETI FEKI.
Mkurugenzi Mtendaji wa HESB, Abdurazack Badru
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESB) imesema haijalishi mnufaika wa mkopo wa elimu ya juu alipatwa na kadhia ya vyeti feki au alifeli shule na kusitishiwa masomo, ilimradi alikopa anatakiwa kulipa deni lake. Aidha, imeeleza kuwa hadi sasa imekwishakusanya Sh 216,992,990,52.98 kati ya Sh 427,708,285,046.48 za mikopo iliyoiva ambayo ipo tayari kukusanywa. Pia imesema licha ya kuendelea kuwatafuta wadaiwa sugu 100,000 kwa sasa, marejesho iliyoyakusanya yameivusha kutoka kwenye lengo ililojiwekea katika mwaka wa fedha 2016/17 la kukusanya asilimia 40 ya mikopo yote iliyoiva.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa HESB, Abdurazack Badru alisema mafanikio hayo yametokana na hatua tatu kuu walizozichukua kuhakikisha marejesho ya mikopo yanafanyika, ambazo ni pamoja na kuwatafuta wadaiwa sugu wa kuanzia mwaka fedha 1994/95.
Alitaja hatua nyingine mbali na kutoa ankara kwa wadaiwa kuwa ni kuwatafuta wanufaika, kupata taarifa zao muhimu pamoja na ukaguzi mahali pa kazi. Kwa mujibu wa Badru, hadi kufikia Juni mwaka huu, wanufaika 139,259 walitambuliwa na kuanza kulipa marejesho ya mikopo yao.
Aliweka wazi kuwa waajiri hasa katika ofisi za umma ndio waliochangia zaidi kupatikana kwa marejesho hayo kwa sababu ya wingi wa watumishi waliokopeshwa ambao kwa namna moja au nyingine ‘wamewabana’ kuhakikisha wanalipa mikopo yao.
“Sekta binafsi nayo imetusaidia ingawa kundi la waliojiajiri mfano kuendesha bodaboda na wanaoendesha kilimo na ujasiriamali mwingine lenye wanufaika 28,893 nalo limerejesha jumla ya Sh bilioni 13.7 na kutuonesha mwitikio mkubwa zaidi,” alieleza.
Aliongeza kuwa bodi hiyo inapitia changamoto nyingi kukusanya marejesho ya mikopo iliyoitoa kwa sababu baadhi ya waajiri hawana taarifa zao zilizokamilika na sahihi huku wengine wakikata marejesho hayo kutoka kwenye mishahara na kutoyawasilisha kwenye bodi hiyo kwa wakati au kutoipeleka kabisa.
Alisema tayari imekwisha wafikisha mahakamani waajiri watatu ambao ni kampuni kwa makosa hayo ya kukaa na fedha za marejesho ya mikopo ilhali wamekwishayatoa kwenye mishahara ya wanufaika ambao ni waajiriwa wao. Kwa maelezo yake, hadi sasa wanawatafuta wadaiwa sugu 100,000.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Featured post
MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO
Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio ...
-
NSIMBO Soko la Katumba Mnyaki linalomilikiwa na halamshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi halina choo tangu kuanzishwa kwake hali...
-
MLELE Shule ya msingi kusa iliyopo katika kijiji cha Kanoge kata ya utende Halmashauri ya wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi inatalajia k...
-
Mahindi MAHINDI yanaendelea kuwadodea wakulima mkoani Rukwa baada ya wafanyabiashara na watu binafsi kuchangamkia mahindi kut...
No comments:
Post a Comment