DAR ES SALAAM
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),
imesema kampuni za simu za mikononi zinaruhusiwa kusajili upya laini kwa
kutumia teknolojia ya kisasa ya kielektroniki inayohusisha uchukuaji wa alama
za vidole.
Kaimu meneja mawasiliano kwa umma wa mamlaka
hiyo, Semu Mwakyanjala amesema walishafanya majaribio kuhusu mfumo huo na kuona
unafaa.
Akizungumzia mfumo huo, meneja uhusiano wa
Airtel Tanzania, Jackson Mmbando amesema kampuni hiyo itaanza kusajili kwa
majaribio.
Amesema baadaye wataendelea kwa wateja
wengine hata ambao walishasajili laini kupitia mfumo wa zamani Lengo ni
kuboresha zaidi mfumo huu.
Chanzo:Mwananchi
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment