Chama cha ACT Wazalendo mkoa wa Katavi kimelaani kitendo cha
uchomaji wa makazi ya watu wanaodhaniwa kuwa wanaishi katika hifadhi ya misitu
na kuitaka serikali kutafakari upya
suala hilo.
Akizungumza na mpanda radio fm mapema leo Katibu wa chama
hicho mkoa wa Katavi Bw Joseph Mona ameiambia mpanda radio kuwa visa vya
uchomaji wa makazi ya wananchi katika vitongoji kadhaa na kuwaacha bila mahali
pakuishi ni suala lisilo kubalika.
Sanjari na hayo ameeleza kuwa mkakati wa chama hicho wa kuishauri
serikali ikiwemo kuikosoa umepelekea kuwasilisha ajenda kadhaa za wananchi
katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jeneral mstaafu Raphael Muhuga kwa ufumbuzi wa tatizo
hilo.
Mwanzoni mwa mwezi huu Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Lilian
Matinga ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya
Mpanda amekili kufanyika kwa zoezi hilo kwa madai kuwa limefanywa katika maeneo
ambayo wananchi wamevamia misitu.
Vitongoji vilivyo kumbwa
na kadhia ya kuchomewa makazi ni Kitongoji cha Nsanda kilichopo kata ya Kanoge,
Makutanio na Mgolokani katika kata ya
Stalike ambapo mamia ya wakazi wanaishi
chini ya miti na familia zao.
#Habari na mwandishi wetu Alinanuswe Edward
No comments:
Post a Comment