Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani Sigmar Gabriel |
Waziri wa
Mambo ya Kigeni wa Ujerumani Sigmar Gabriel amesema Uturuki haitawahi kuwa
mwanachama wa Umoja wa Ulaya kama itaendelea kuongozwa na Recep Tayyip Erdogan.
Katika
mahojiano yaliyochapishwa kwenye gazeti la Bild, nchini Ujerumani, Gabriel
amesema rais huyo wa Uturuki ameshindwa kuyapa umuhimu mazungumzo ya nchi hiyo
kujiunga na Umoja wa Ulaya.
Matamshi
yake huenda yakayadhoofisha hata zaidi mahusiano kati ya Ujerumani na Uturuki
ambayo yamezorota kutokana na masuala kadhaa. Ujerumani ina wasiwasi kuwa
mamlaka mapana aliyopewa Erdogan kupitia kura ya maoni mwezi Aprili yanaisogeza
Uturuki mbali na misingi ya kidemokrasia.
Viongozi
wa Umoja wa Ulaya wanakosoa msako wa Erdogan dhidi ya wapinzani kabla na baada
ya jaribio lililoshindwa la mapinduzi dhidi yake Julai mwaka jana.
Erdogan anasema msako
huo pamoja na mamlaka yake mapana vinahitajika ili kusaidia Uturuki kupambana
na changamoto kubwa za kiusalama ndani na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment