Kaimu Kamanda wa Polisi
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya
|
Dar es Salaam.
Kaimu Kamanda wa
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya amethibitisha kushambuliwa
ofisi za wanasheria za IMMMA saa 8 usiku wa kuamkia leo Jumamosi, Agosti 26.
Mkondya amesema polisi
wanafanya uchunguzi kujua ni nini kilihusika katika tukio hilo la mlipuko.
“Tupo hapa eneo la tukio,
uchunguzi unaendelea na ukikamilika tutawapa taarifa zaidi, ila hatujajua kama
bomu limehusika,” amesema Mkondya.
Ameeleza hadi sasa hakuna
watu wanaoshikiliwa kuhusika na tukio hilo.
Mmoja wa viongozi wa
Kampuni ya IMMMA, Sadock Magai amesema hakuna wizi ambao umefanyika katika mali
zilizokuwa ndani.
“Tuwaachie Jeshi la Polisi
wafanye kazi yao,” amesema Magai.
Ofisi za wanasheria
wa kampuni hiyo zipo Barabara ya Umoja wa Mataifa eneo la Upanga jijini hapa.
Miongoni mwa wamiliki
wa kampuni hiyo ni Fatma Karume, ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu wa Zanzibar,
Amani Abeid Karume.
No comments:
Post a Comment