MONROVIA
Rais mpya wa Liberia George
Weah amemfuta kazi Waziri wa Sheria,Charles Gibson baada ya malalamiko kuwa
amepokonywa leseni ya uwakili baada ya kumtapeli mteja wake.
Kabla ya uteuzi wake,Gibson
amepatikana na hatia hiyo na Mahakama ya Juu baada ya kumtapeli mteja wake Dola
za Marekani elfu 25 na kuagizwa kuzirejesha.
Rais Weah amemteua Musa Dean
aliyekuwa Wakili katika Tume ya Uchaguzi kuchukua nafasi hiyo.
Mwanasoka huyo nyota wa wa
zamani wa Liberia alichaguliwa kuwa Rais na kuchukua nafasi ya Bi.Ellen Johnson
Sirleaf ambaye alikuwa Rais wa kwanza mwanamke barani Afrika kuchaguliwa
kidemokrasia ambaye alikabidhi madaraka kwa amani.
Chanzo:EATV
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment