Mkuu wa Wilaya ya Mpanda katika Mkoa wa Liliani Charles Matinga |
MPANDA
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda katika Mkoa wa Liliani
Charles Matinga amewataka wazazi na wanachi kwa ujumla kuendelea kushiriki
vyema katika shughuli za kuchangia miundombinu ya Elimu.
Matinga ametoa wito huo katika kikao cha kamati ya
ushauri wilaya ya Mpanda kilichofanyika manispaa ya Mpanda. amesema ni wajibu
kwa kila mwananchi kushiriki ipasavyo katika shughuli za maendeleo ya elimu kwa
kuzingatia utaratibu uliotolewa wa kuhusu yote ya hiari kwa wananchi kupitia
ofisi ya mkurugenzi.
Matinga amewataka kushiriki kwa
kuzingatia waraka uliotolewa na Ofisi ya Rais
Tawala za mikoa na serikari za mitaa
Tamisemi kwa halmashauri zote nchini kuhusu utaratibu wa michango
shuleni kote nchini.
Katika hatua nyingine Matinga amewaagiza wakurugenzi
kusambaza waraka huo kwa maafisa wa kata pamoja na maafisa maendeleo ya jamii
ili wawaelimishe wananchi kuhusu tamko la michango shuleni ili kuondoa
mkanganyiko unaojitokeza kwa wananchi kuhusu suala la michango shuleni.
Kikao hicho kilichokuwa
na lengo la kupitia rasimu ya bajeti kwa mwaka 2018/2019 kimeshirikisha
Halmashauri zote mbili za Wilaya ya Mpanda.
Chanzo:Paul Mathias
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment