Wakazi
wa kijiji cha Mtakuja kilichopo Halmashauli ya wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi
wamesema,ukosefu wa soko la kuuza bidhaa wanazozalisha shambani kunasababisha
waendelee kuwa maskini.
Wakazi
hao wamesema kwa sasa wanalazimika kuuza kwa kuzungunguka mitaani kutokana na
kutokuwepo kwa soko hilo.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Mtakuja Bw.Daud Peter Nyasio amekiri
kuwepo kwa tatizo la ukosefu wa soko huku akisema kuna mikakati ya kuanzisha
soko la kijiji pamoja na soko la kata ya Kapalala litakalohudumia vijiji vitatu
vya kata hiyo.
Kijiji
cha Mtakuja kina zaidi ya wakazi elfu tatu waliopo katika vitongoji vya
Igonda,Mtakuja B,Mbugani,Bombani na Tenkini ambapo wengi wao hujishghulisha na
kilimo cha mazao mbalimbali yakiwemo mahindi,karanga na tumbaku.
Chanzo:Isaack Gerlad
No comments:
Post a Comment