Wananchi wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi
wameiomba serikali kutoa elimu juu ya umuhimu wa mwenge wa uhuru katika
kuhamasisha maendeleo.
Wamebainisha hayo wakati wakizungumza na Mpanda
Radio na kusema kuwa elimu inapaswa itolewe kwa wananchi kuhusu mwenge na
kushauri kuangalia msimu kwani mkoani hapa kipindi cha masika huwa ni
changamoto hivyo huwawia vigumu hata katika kushughulikia fursa za kujitafutia
kipato.
Aidha Mwenge wa uhuru utakagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani katavi.
Tarehe 2 mwezi wa tano Halmashauri ya Manspaa ya Mpanda inatarajia
kupokea Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa ndege na mkesha utafanyika katika
viwanja vya shule ya msingi Kashato huku kauli mbiu kwa mwaka huu ikiwa ni elimu ni ufunguo wa
maisha wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa.
Chanzo:Johar Secky
No comments:
Post a Comment