Madereva
bajaji Manispaa ya Mpanda wameilalamikia mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa nchi
kavu na majini SUMATRA kwa kutotoa mrejesho wa kutopewa namba za usajili licha
ya kukamilisha vigezo vyote vinavyotakiwa.
Wamesema
hayo wakati wakizungumza na mpanda radio na kueleza kuwa zoezi hilo la ugawaji
namba za usajili na kupewa vituo rasmi limesimama ghafla bila kupewa taarifa
yoyote.
Kwa upande
wake Meneja wa Udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini
Sumatra Mkoa wa Katavi Amani Mwakalebela amesema kuwa zoezi la ugawaji
namba kwa bajaji litaendelea baada ya stendi kuu ya mabasi kukamilika.
Stendi kuu
ya mabasi yaendayo mikoani ambayo ipo katika hatua ya mwisho inatajwa kuwa
miongoni mwa stendi za kisasa nchini Tanzania ikiunganishwa pamoja na fulsa kwa
wafanyabiashara.
Chanzo:John
John
No comments:
Post a Comment