Wednesday, 17 January 2018

TRA katika Halmashauri ya manispaa ya Mpanda imekusanya mapato kufikia 78% tofauti na ilivyo kuwa mwezi wa kumi na moja mwaka jana.


MPANDA

Makusanyo yamapato katika Halmashauri ya manispaa ya Mpanda yameongezeka nakufikia 78% tofauti na ilivyo kuwa mwezi wa kumi na moja mwaka jana ambapo walikusanya shilingi milioni 370.

Hayo yamebainishwa na Afisa Mapata wa manispaa  ya Mpanda  Mola Elias Wakati akizungumza na Mpanda Redio ambapo ameeleza kuwa zaidi ya shilingi milioni 480 Katika kipindi cha mwezi wa 12/ 2017 zimeweza kupatikana.

Aidha Mola amesema kumekuwepo na changamoto kwa baadhi ya wafanyabiashara kuwa wazito katika kutoa kodi na kuwaommba kujenga tabia ya kulipa kodi hali ambayo itasaidia kukuza uchumi wa taifa kwa ujumla

Kwa upande wafanyabiashara katika manispaa ya Mpanda wamesema kulipa kodi ni wajibu wa kila mwananchi ili kuisaidia serekali kupata fedha kwa ajili ya kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo. 


Chanzo: Paul Mathius

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...