Thursday, 18 January 2018

Marekani jana imetangaza kuwa itazuia kiasi cha dola milioni 65 zilizokuwa zimepangwa kulifadhili shirika la Umoja wa mataifa linalowahudumia wakimbizi wa Palestina la UNRWA.


WASHINGTON

Marekani jana imetangaza kuwa itazuia kiasi cha dola milioni 65 zilizokuwa zimepangwa kulifadhili shirika la Umoja wa mataifa linalowahudumia wakimbizi wa Palestina la UNRWA, wiki mbili baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutishia malipo ya baadaye.

 Wizara hiyo imesema Marekani itatoa dola milioni 60 kati ya milioni 125 zilizopangwa awali, lakini zilizobaki zitazuiwa kwa sasa.

Maafisa wa Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani wamesisitiza uamuzi huo haukuchukuliwa ili kuwashinikiza viongozi wa Palestina, lakini kwa sababu Marekani inataka nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa zisaidie kulipa na kurekebisha shirika la UNRWA.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema hakuwa na taarifa ya uamuzi huo wa Marekani, lakini taarifa alizozisikia zimempa wasiwasi sana.


Chanzo:Bbc swahili

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...