Waziri wa Elimu, Profesa. Joyce Ndalichako |
DAR ES SALAAM
Waziri
wa Elimu, Profesa. Joyce Ndalichako amesema kuwa serikali itagharamia
shughuli za mazishi ya Mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji
(NIT), Akwiilina Akwiline ambaye ameuawa kwa kupigwa risasi Februari 16, 2018 eneo
la Mkwajuni DSM.
Waziri
Ndalichako amesema kuwa viongozi mbalimbali wameguswa na kifo hicho kwani
mwanafunzi huyo hakuwa na hatia yoyote na kusema kifo chake ni pigo kubwa kwa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ndalichako
amedai kuwa kifo cha mwanafunzi huyo kimetokea wakati akiwa kwenye harakati ya
kupeleka barua ya maombi ya mafunzo kwa vitendo ambayo alikuwa akitegemewa
kuanza Februari 26, 2018 na kudai kifo hicho kimezima ndoto yake.
Aidha
Kwa mujibu wa kamanda wa Kanda maalamu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa
amesema maafisa sita wa polisi
wamekamatwa kuhusiana na kifo cha mwanafunzi huyo.
Chanzo:Mwananchi
No comments:
Post a Comment