KATAVI
Wafanyabiashara
mkoani Katavi wameiomba mamlaka ya
mapato TRA kutoa elimu juu ya ulipaji kodi na matumizi ya mashine za
kielektronic EFD ili kuondokana na
migogoro isiyo ya lazima.
Hayo
yamesemwa katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Idara ya maji ambapo
wafanyabiashara wametaja sababu za kutolipa kodi kuwa ni ukosefu wa elimu juu
ya matumizi ya mashine hizo.
kamishna
mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania TRA
Bw Charles Edward Kichele amewataka viongozi wa TRA mkoa
kuhakikisha wafanyabiashara waliolipia
mashine kupatiwa kwa wakati na kuagiza kuwa wafanyabiashara ambao tayari
wamelipia mashine na hawajapata wasisumbuliwe kwani ni wajibu wa mamlaka hiyo .
Mashine za Risiti za Kielektroniki ni mashine
zilizotengenezwa kwa ajili ya kutumika katika biashara kwa ajili ya kudhibiti
usimamizi kwa ufanisi katika maeneo ya uchambuzi wa mauzo na mfumo wa udhibiti
wa mali .
Chanzo:Adelina Erenest
No comments:
Post a Comment