Barabara zinazotengenezwa mkoani Katavi |
Mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga amewataka mawakala wa barabara kushirikiana na halmashauri zote kuweza kubuni na kuboresha barabara mpya zitakazo saidia kukuza uchumi mkoan katavi.
Aliyasema
hayo katika kikao cha 11 cha utekelezaji wa matengenezo ya barabara kwa mwaka
2017/2018 na mapendekezo ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2018/2019"halmashauri ndizo zinazotambua swhemu ambazo zinauhitaji zaidi"alisema Muhuga.
Mkuu wa Mkoa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Rafael Muhuga |
Kaimu Meneja Tanroads Mkoa wa Katavi Mhandisi MARTIN MWAKABENDE alisema kuwa katika mwaka wa
fedha 2018/19 wakala wa barabara mkoa wa katavi waliomba kutengewa jumla ya shilingi
bilion 15.1 kwa ajili ya kulipa fidia,kufanya ukarabati wa barabara,kufanya
usanifu wa kina na kujenga madaraja.
Ubovu
wa miundombinu hususani barabara na madaraja mkoani katavi ni kikwazo kikubwa
cha maendeleo kwa wananchi'
No comments:
Post a Comment