Watoto wakipata elimu |
Wananchi
katika halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamesema kutokuwepo kwa
mabaraza ya watoto katika ngazi ya kata kunachangia kuwepo kwa vitendo vya
unyanyasaji kwa watoto katika jamiii.
Wamesema
kuwa vitendo vya ukandamizaji dhidi ya watoto vimekuwa vikiongezeka kila mwaka
kutokana na kunyimwa fursa kuelezea changamoto na maswaibu mbalimbali
wanayokabiliana nayo.
Katika
hatua nyingine wananchi hao wamezitaka mamlaka zinazo husika kuaandaa semina
elimishi kuhusu umuhimu wa kuyatambua mabaraza hayo na kufahamishwa juu ya
utendaji wake .
Maafisa
wa maendeleo ya jamii manispaa ya Mpanda hawakutoa ushirikiano kuhusu kueleza uwepo wa mabaraza hayo ngazi
ya kata .
Sera
ya Maendeleo ya Mtoto ya Mwaka 2008 imeanisha tamko la Sera kuhusu uanzishwaji
mabaraza hayo katika ngazi mbalimbalina
ikizingatiwa kuwa mabaraza hayo
ni sehemu ya utekelezaji wa sheria ya Mtoto namba 21 ya Mwaka 2009.
Source: Paul mathias
No comments:
Post a Comment