wanafunzi rungwa sekondari |
Wanafunzi
wa shule ya sekondari Rungwa katika
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi ,wamesema kuwepo kwa maabara
shuleni hapo kumewasaidia kufanya vizuri katika masomo ya sayansi.
Wanafunzi
hao wakiwemo Nichoraus Ntagaye,Hagma Shabaani na Sekela Laurence wameiambia
Mpanda Radio kuwa,masomo ya sayansi yamekuwa rahisi kwa sababu ya kujifunza kwa
vitendo.
pichani ni maabara ya wanafunzi kujifunzia |
Mwalimu
Martin Songolo wa Kemia na Baiolojia
katika shule hiyo amesema pamoja na uhaba wa vifaa katika maabara ufundishaji
umekuwa rahisi kuliko kufundisha kwa nadharia.
Deus
Kazonde ambaye ni mwalimu mwandamizi
taaluma katika shule hiyo amesema ufaulu kwa kidato cha nne kwa mwaka 2017 ulikuwa asilimia tisini
tofauti na miaka iliyopita.
Source: Issack gerald
No comments:
Post a Comment