Wednesday, 21 February 2018

Mkazi wa kata ya Inyonga Halmashauri ya Wilaya ya Mlele anayefahamika kwa jina la Amani Silveri Pendelesi amefikishwa mahakamani kwa kosa la kuingia nchini bila kuwa na vibali maalumu.


MLELE

Mkazi wa kata ya Inyonga Halmashauri ya Wilaya ya Mlele anayefahamika kwa jina la Amani Silveri Pendelesi amefikishwa mahakamani kwa kosa la kuingia nchini bila kuwa na vibali maalumu.

Tukio hilo limetokea tarehe 14 mwezi huu katika kata ya inyonga  mtuhumiwa mwenye umri wa miaka 35 raia wa Burundi  amekamatwa wakati akijaribu kujipatia kitambulisho cha uraia wa Tanzania ambacho ni kinyume cha sheria za nchi hii..

Kesi hiyo imesikilizwa leo katika Mahakam ya hakimu mkazi mkoani katavi mbele ya hakimu Omari Hassani Kingwele na mwendesha mashtaka wa uhamiaji Joseph Bajagae na mshitakiwa kukiri kutenda kosa hilo.

Hata hivyo mshitakiwa huyo amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela au kutoa faini ya shilingi laki tano za kitanzania.

Kuingia  nchini bila kibali ni kinyume na kifungu cha 45 sehemu ya kwanza cha sheria ya uhamiaji na ukurasa wa saba sura ya 54 kama ilivyofanyiwa mabadiliko mwaka 2016 imehukumu kesi hiyo.

Chanzo:Furaha Kimondo      

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...